Mahadhi aahidi kuendeleza makali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2018
Mahadhi aahidi kuendeleza makali
Baada ya juzi kuifungia timu yake bao pekee kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis ya Shelisheli, mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi, amesema bao hilo litamfungulia akaunti ya mabao kwenye michuano hiyo msimu huu.

Bao hilo la dakika ya 67 liliiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa 1-0 katika Uwanja wa Taifa na kujiweka matumaini ya kusonga mbele.

Mahadhi aliyeimarisha kiwango chake tangu kuanza kwa mwaka 2018 amesema kuwa amejisikia furaha kuifungia timu yake bao pekee katika michuano hiyo.

"Nimefurahi sana, ndoto yangu ni kuendelea kuifungia Yanga kwenye michuano hii," alisema Mahadhi.

Aidha, alisema licha ya ushindi huo wa bao moja, ana uhakika timu yake itawan'goa wapinzani wao hao kutoka Shelisheli

"Tunajipanga kwa mchezo wa marudiano, naamini tutasonga mbele, " alisema Mahadhi.

Mahadhi aliichangamsha safu ya ushambuliaji ya Yanga katika mchezo huo baada ya kuingia kwenye dakika ya 64 kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib.

Mashabiki wengi wa Yanga wanatamani kumuona mshambuliaji huyo akipata nafasi zaidi kwenye kikosi cha Yanga kutokana na kasi yake kuwasumbua walinzi wa timu pinzani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’