Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ataangalia afya za nyota wake Khalid Aucho na Jesus Moloko katika program za mwisho za mazoezi kuona kama anaweza kuwatumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zalan Fc siku ya Jumamosi
Aucho na Moloko walipata majeraha kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0
Aucho anaweza kuwa mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga mpaka sasa msimu huu
Nabi amemtumia katika kila mchezo kuanzia ule wa Ngao ya Jamii ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba
Alipata majeraha ya nyama za paja katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, majeraha ambayo yanaweza kumuweka nje hadi wiki mbili

Moloko amekuwa na mchango mkubwa katika mechi alizoshiriki pamoja na kuwa changamoto ya majeraha imemuandama sana
Aina ya uchezaji wake inamfanya kuwa mchezaji anayefanyiwa rafu zaidi na hivyo kuumia mara kwa mara