Mkurugenzi wa Soka la Vijana Yanga Mwinyi Zahera amethibitisha kuwa klabu ya Olympic Marseille inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa inamuhitaji mshambuliaji Clement Mziza kwa ajili ya kufanya majaribio
Zahera amesema tayari Marseille wameshatuma mwaliko wa kinda huyo kutakiwa kwa majaribio ya wiki mbili yatakayofanyika nchini Ufaransa.
Hivi karibuni Mawakala kutoka Ufaransa walikuwa Tanzania kushuhudia michuano maalum ya vijana U20 iliyowashirikisha mabingwa wa Ufaransa (U20) Monpellier
Michuano hiyo ilifanyika baada ya kumalizika kwa Ligi ya U20 Mziza akionyesha kiwango bora akifunga mabao saba na kuwa mfungaji bora
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alimjumuisha Mziza kwenye kikosi chake msimu huu juzi akipata nafasi ya kucheza katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar
"Huo mwaliko upo klabuni viongozi wanaufanyia kazi nafikiri katika majaribio hayo atafanikiwa kwa kuwa nimekuwa naye naona ubora wake kwa umri wake Marseille hawataweza kumuacha," alisema Zahera