Kisinda ataongeza ubora kwenye kikosi - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Sep 2022
Kisinda ataongeza ubora kwenye kikosi - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameeleza kufurahishwa na urejeo wa winga Tuisila Kisinda aliyejiunga na Yanga akitokea klabu ya RS Berkane

Yanga ilimuuza Kisinda RS Berkane klabu aliyoitumikia kwa msimu mmoja kabla ya Yanga kumrejesha siku ya mwisho ya dirisha la usajili August 31 2022

Nabi amesema Kisinda ataongeza kitu katika kikosi chake akiamini kuwa ataendeleza ubora wake aliokuwa nao kabla ya kuondoka Yanga

"Nimefurahi Kisinda kurejea Yanga, ni mchezaji mzuri ambaye ataongeza ubora katika kikosi. Naamini ataendeleza ubora wake aliokuwa nao kabla ya kuondoka," alisema Nabi

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zalan Fc, Nabi amesema pamoja na wachezaji wake kukabiliwa na uchovu, wako tayari kwa mchezo huo

"Tumecheza mechi mfululizo, jambo hili limetuletea maumivu na uchovu. Kuna baadhi ya wachezaji kama Khalid Aucho, Morrison, Djuma Shaban hatutaweza kuwatumia kutokana na majeraha waliyopata"

"Hata hivyo Yanga ni klabu kubwa na muhimu zaidi wachezaji wanafahamu wanacheza michuano mikubwa ya ligi ya mabingwa. Watakuwa tayari kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’