Matchday : Yanga vs Zalan Fc, CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2022
Matchday : Yanga vs Zalan Fc, CAF CL

Baada ya ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza, leo Yanga inakwenda kukamilisha mchezo wa mkondo wa pili michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Zalan Fc kutoka Sudan Kusini

Mchezo huo utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja kamili usiku

Ili kufuzu raundi ya kwanza, Yanga inahitaji ushindi, sare au hata kufungwa sio zaidi ya mabao matatu

Hata hivyo Yanga hawatarajii kupoteza mchezo huo mbele ya mashabiki wao pamoja na kuwa wakati mwingine mpira unaweza kuwa na matokeo ya kikatili

Yanga ilidhihirisha ubora wake kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza na matarajio ya wengi ni kuona wanaendeleza pale walipoishia katika mchezo huo ambao mshambuliaji Fiston Mayele alifunga mabao matatu 'hat-trik'

Kuelekea mchezo wa leo, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amebainisha kuwa atafanya mabadiliko madogo katika kikosi chake akiwakosa baadhi ya wachezaji ambao walipata majeraha kwenye michezo iliyopita

Nyota watatu Khalid Aucho, Djuma Shabani na Bernard Morrison hawatakuwa sehemu ya mchezo Nabi akibainisha nafasi zao ataweka wachezaji wengine

Mashabiki wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ambao Yanga ni mwenyeji, viingilio ni rafiki ambapo mzunguuko ni Tsh 2,000/- tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’