Ni siku kubwa, siku maalum kwa Wananchi kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Zalan Fc
Yanga inahitaji matokeo leo ili kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambayo itawahakikishia tiketi mbili mkononi
Katika raundi ya kwanza Wananchi watakuwa na nafasi ya kutinga hatua ya makundi kama watapata matokeo ya ushindi katika michezo ya raundi hiyo au kuhamishiwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho (kama watashindwa) ambako watakuwa na nafasi ya kutinga hatua ya makundi kama wataibuka na ushindi pia
Hivyo mchezo dhidi ya Zalan Fc leo una umuhimu mkubwa. Yanga iko mbele kwa mabao 4-0 lakini ina dakika nyingine 90 za kuhakikisha matokeo ya ushindi kwa ujumla yanapatikana
Itakuwa heshima kubwa kwa Yanga kushinda mbele ya mashabiki wao wakiwa wameujaza uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Zalan Fc hawana cha kupoteza baada ya kubuguzwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza
Lakini kwa vyovyote vile, Zalan Fc hawapaswi kutoka salama hapo Lupaso....!