Baada ya ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Zalan Fc, Wananchi wakitinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, kutakuwa na takribani siku 10 za mapumziko kupisha michezo ya Kimataifa iliyo kwenye kalenda ya FIFA
Mchezo utakaofuata ni wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa Septemba 29 mkoani Mbeya
Pengine huu utakuwa mchezo wa kwanza mashabiki wa Yanga kumshuhuidia winga Tuisila Kisinda aliyerejea kutoka klabu ya RS Berkane
Kisinda amepata leseni inayomruhusu kushiriki mechi za ligi kuu na kombe la FA wakati akisubiri Yanga itinge hatua ya makundi ligi ya mabingwa/Shirikisho aweze kushiriki kwenye michuano hiyo ya CAF
ADVERTISE HERE