Kikosi cha Yanga kimeweka kambi ya muda mfupi katika Hotel ya Zimbo jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 18 dhidi ya Majimaji.
Mchezo huo unatarajiwa kuupigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Taifa.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wanauchukulia mchezo huo kwa uzito kwa kuwa Majimaji ni moja ya timu bora kwenye ligi.
Aidha matokeo ya ushindi yataendelea kuipa presha Simba iliyo kileleni kwa tofauti ya alama saba.
Baada ya Azam FC kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar jana huku Singida United ikilazwa bao 1-0 na Stand United juzi, ni Yanga pekee yenye nafasi ya kuikaribia Simba kama itapata ushindi kwenye mchezo huo.
Simba itashuka dimbani keshokutwa kuumana na Mwadui FC mkoani Shinyanga.
Ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wake Yanga inalazimika kushinda kila mchezo huku ikiiombea Simba iangushe pointi.

ADVERTISE HERE