Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Mali kitakachocheza mechi za Kimataifa za kirafiki dhidi ya Zambia
Aidha kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki yeye amejumishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Burkina Faso ambayo itacheza na DR Congo
Nyota hao wanaungana na Kibwana Shomari, Dickson Job na Feisal Salum 'Fei Toto' ambao wamejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itakayoshiriki michuano maalum itakayofanyika Libya ikizihusisha nchi za Libya (wenyeji), Uganda na Tanzania




ADVERTISE HERE