Safu ya ushambuliaji Yanga kuongezewa makali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2022
Safu ya ushambuliaji Yanga kuongezewa makali

Pamoja na ushindi wa mabao 5-0 ambao Yanga walipata dhidi ya Zalan Fc na kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-0, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi hakufurahishwa na wachezaji wake katika eneo la ushambuliaji wakipoteza nafasi nyingi

Katika mechi zote dhidi ya Zalan Fc, Yanga ilifunga mabao yote kwenye kipindi cha pili lakini nafasi nyingi zaidi zilitengenezwa katika kipindi cha kwanza lakini hazikutumika

Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki Yanga inarejea mazoezini kujiandaa na mechi zinazofuata kwenye ligi kuu lakini pia mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema watafanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika mchezo dhidi ya Zalan, muhimu zaidi kuongeza umakini kwa washambuliaji ili waweze kutumia nafasi

"Ni kweli tungeweza kufunga mabao mengi zaidi katika mchezo dhidi ya Zalan Fc lakini tulipoteza nafasi nyingi. Hili sio jambo zuri kwa sababu zipo mechi tunaweza tusipate nafasi nyingi hivyo tunapaswa kutumia nafasi ipasavyo," alisema Kaze

Yanga inakabiliwa na michezo miwili ya ligi kuu ambayo itapigwa ugenini dhidi ya Ihefu Fc (Sept 29) na Ruvu Shooting (Oct 03) kabla ya mchezo wa mkondo wa kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Oct 7-9 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’