Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Burkina Faso inayotarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki katika kalenda ya FIFA
Kesho Ijumaa, Sept 23 Burkina Faso watacheza na DR Congo na watashuka tena dimbani Jumanne Sept 27 kuwakabili Comoro
Aziz Ki, mlinda lango Djigui Diara (Mali) ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa

Wengine ni Kibwana Shomari, Dickson Job na Feisal Salum 'Fei Toto' ambao wako timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Aboutwalib Mshery, Clement Mziza na Denis Nkane wao wako kwenye kikosi cha timu ya Taifa U23
ADVERTISE HERE