Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi imemfungia mechi tatu winga wa Yanga, Bernard Morrison kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa Azam Fc, Lusajo Mwaikenda katika mechi ya Yanga dhidi ya Azam katika uwanja wa Mkapa
Morrison pia atalipa faini ya Tsh Milioni 1. Kamati hiyo ya saa 72 imetoa taarifa leo siku 16 baada ya mchezo husika!
Adhabu hiyo itamfanya Morrison akose mechi dhidi ya Simba ambayo itapigwa Oktoba 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Morrison atakosa mechi dhidi ya Ruvu Shooting, Namungo Fc na Simba
Kama adhabu hiyo ingetolewa kabla ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, au mchezo dhidi ya Ihefu Fc usingesogezwa mbele, Morrison angeweza kuwa na nafasi ya kucheza mchezo dhidi ya Simba
Adhabu hii ni wazi itarejesha ule mjadala kuwa Kamati hiyo imekuwa haipati kigugumizi kuadhibu makosa yanayofanywa na wachezaji wa Yanga lakini ni kinyume pale makosa yanapofanywa na timu nyingine...!