Iwe Jua, iwe mvua

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2022
Iwe Jua, iwe mvua

Wananchiiiiiiii.. Oktoba 08 ni siku muhimu kwa klabu ya Yanga, mchezo wa mkondo wa kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni siku muhimu kwa sababu Yanga inahitaji kupata ushindi mnono siku hiyo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga makundi ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni takribani miaka 24 imepita tangu Yanga icheze makundi ya ligi ya mabingwa, msimu huu Wananchi wana nafasi ya kurejea katika hatua hiyo kibabe

Kikosi bora, benchi bora la ufundi, uongozi bora na mashabiki bora! Huu ni mwaka wa Wananchi

Mhamasishaji wa mashabiki wa Yanga Haji Manara ametangaza kauli mbiu itakayotumika kuelekea mchezo huo, IWE JUA, IWE MVUA

Yanga itakuja na utaratibu maalum kwa ajili ya mashabiki ambao wataingia uwanjani kwa kazi maalum ya kushangilia na sio kutazama mpira tu

Wewe Mwananchi ambaye unahitaji kuona anga inatinga makundi msimu huu unapaswa kuwa tayari kuingia uwanjani KUSHANGILIA

Yanga pia imejipanga kwenda na mashabiki wake kwenye mchezo wa marudiano kule Sudan, uongozi umeahidi kutangaza utaratibu wa safari mapema

Ni hivi, IWE JUA, IWE MVUA lazima kieleweke...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’