Morrison ametoka, Kisinda ameingia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Sep 2022
Morrison ametoka, Kisinda ameingia

Winga Bernard Morrison hatashiriki michezo mitatu ijayo ya ligi kuu ya NBC baada ya kufungiwa na Bodi ya Ligi kwa kosa alilofanya katika mchezo dhidi ya Azam Fc Septemba 06

Habari njema kwa Yanga ni kuingia kikosini kwa winga Tuisila Kisinda ambaye usajili wake uliidhinishwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji licha ya kuwekewa ngumu na TFF hapo awali

Kisinda anatarajiwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na pengine Oktoba 03 atacheza mchezo wa kwanza wa ligi tangu arejee dhidi ya Ruvu Shooting

Ataungana na Mcongomani mwenzake Jesus Moloko ambaye kiwango chake kimeimarika mara dufu tangu msimu huu ulipoanza

Lakini pia Yanga ina Farid Mussa ambaye msimu huu ameendelea kuwaduwaza Wananchi kwa ubora anaoonyesha katika michezo ya hivi karibuni

Farid amehusika kwenye mabao matatu katika michezo miwili iliyopita pia akifunga bao katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zalan Fc

Pamoja na kuwa Morrison atakosa michezo mitatu inayofuata kwenye ligi, adhabu yake haihusiani na michuano ligi ya mabingwa hivyo huko ataendelea kuwakimbiza

Morrison amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa na sasa anaendelea na mazoezi makali kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal, Oktoba 08

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’