Leo klabu ya Yanga imetimiza mwaka mmoja na siku moja bila ya kupoteza mchezo wowote wa mashindano rasmi (sio mechi za kirafiki)
Septemba 25 mwaka jana katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba na tangu wakati huo hawajapoteza mchezo wowote mpaka leo
Alama 10 kileleni mwa msimamo wa ligi msimu huu, wakishinda michezo mitatu na kutoa sare mchezo mmoja.
Ligi ya mabingwa hatua ya awali wakishinda michezo miwili dhidi ya Zalan FC. Msimu uliopita walicheza michezo 30 ya ligi pasipo kupoteza.
Katika msimu huo pia walicheza michezo mitano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na walimaliza pasipo kupoteza mchezo wowote, licha ya kukutana na upinzani mkali kwenye mchezo wa fainali waliocheza na Coastal Union na kushinda kwa mikwaju ya penati.
Yanga mara ya mwisho walipoteza mchezo 25 April 2021 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu
Huo ndio mchezo pekee ambao kocha Nasreddine Nabi amepoteza kwenye ligi kuu tangu alipojiunga na Yanga mwanzoni mwa April 2021
Yanga imecheza mechi 41 mfululizo pasipo kupoteza katika ligi kuu!