Wakati wowote Yanga itatangaza safu mpya ya viongozi watakaojaza nafasi mbalimbali za sekretarieti, imeelezwa Yanga tayari imemleta Mtendaji Mkuu
Yanga inatarajiwa kumtangaza Andrey Mtine kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu akitokea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo
Tangu kuondoka kwa Senzo Mazingisa, nafasi ya Mtendaji Mkuu imekuwa ikikaimiwa na Simon Patrick ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama
Ni suala la muda tu utambulisho wa Mzambia huyo pamoja na wenzake katika nafasi mbalimbali
Miongoni mwa majina mengine yanayotajwa ni Afisa Habari, mchambuzi wa Azam TV, Ali Kamwe akichomoza kwa mara nyingine
ADVERTISE HERE