Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi hataki kuona wachezaji wake wanafanya makosa yanayopelekea kuadhibiwa na hivyo kuigharimu timu
Kocha huyo raia wa Tunisia na Ubelgiji, hakufurahishwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu winga Berbard Morrison ambaye atakosa mechi dhidi ya Ruvu Shooting, Namungo Fc na Simba
pamoja na kuwa zipo nyakati wachezaji wake 'wanachokozwa' au kutotendewa haki kwenye baadhi ya matukio, Nabi amesema atafanya mazungumzo maalum nao ili kuhakikisha wanakuwa watulivu
"Nitakaa na wachezaji wote, ni lazima tuzungumze kama familia moja, kuna wakati ukiona jirani yako anawaumiza sana watoto wako, ni vyema ukakaa chini na watoto wako na kuzungumza nao"
"Kitu bora hapa ni sisi wenyewe kujiweka salama kwanza, licha ya kwamba na wao wanaumizwa sana, hatuna namna zaidi ya kuwa wapole na kutofanya vitu vitakavyotuumiza zaidi," Nabi amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
Kabla ya tukio la Morrison ambaye alimkanya mchezaji wa Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 06, kulikuwa na mfululizo wa matukio yasiyo ya kiungwana ambayo walifanyiwa wachezaji wa Yanga pasipo hatua zozote kuchukuliwa
Nabi anahitaji kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia ili wasiingie katika mtego wa kuadhibiwa kwani ni wazi matukio yanayofanywa na wachezaji wa Yanga yanaonekana haraka na hatua huchukuliwa mara moja