Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jana ilihitimisha mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao Libya katika mchezo ambao walipoteza kwa mabao 2-1
Tanzania ilicheza michezo miwili ya kirafiki huko Libya ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda Cranes
Wachezaji wa Yanga Kibwana Shomari na Dickson Job walikuwa sehemu ya kikosi hicho huku Feisal Salum 'Fei Toto' akibaki jijini Dar es salaam baada ya kupata majeraha katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Zalan Fc

Kibwana na Job sasa wanarejea katika kikosi cha Yanga kuungana na wenzao wanaoendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Oktoba 03
Aidha mlinda lango Djigui Diarra nae anatarajiwa kutua nchini wakati wowote baada ya kumaliza majukumu ake katika timu ya Taifa ya Mali
Yanga pia ilikuwa na wachezaji katika timu ya Taifa ya vijana U23 Aboutwalib Mshery, David Bryson, Denis Nkane na Clement Mziza ambao tayari wamerejea nchini kutokea Rwanda walikoisaidia Ngorongoro Heroes kufuzu raundi ya kwanza kusaka tiketi ya michuano ya Afcon 2023 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Sudan Kusini