Mabadiliko ya kweli ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga, mchakato wake uliendeshwa kwa uwazi na sasa matunda yake yameanza kuonekana
Tumeshuhudia usajili makini ukifanywa na Yanga kwa kushirikiana na GSM katika msimu uliopita na maboresho mengine kufanyika msimu huu
Leo hii Wananchi wanajivunia kwani timu yao imecheza mwaka mzima pasipo kupoteza mchezo rekodi ambayo hakuna klabu imewahi kuiweka hapa nchini
Sio ajabu Yanga inaweza kuwavutia kina Andrey Mtine (CEO) ambaye amewahi kufanya kazi katika taasisi kubwa kama TP Mazembe
Mwezi August Kocha maarufu Pitso Masemane alivutiwa na 'parade' ya kusherehekea ubingwa iliyofanywa na Yanga na akafunga safari kuja kushuhudia wiki ya Mwananchi
Sasa Mosemane ni balozi mzuri wa klabu ya Yanga na hata katika kurasa zake za mitandao ya kijamii amekuwa akishiriki mijadala mbalimbali inayohusiana na Yanga
Dhamira ya viongozi wa Yanga ni kuona wanakidhi kiu na matamanio ya Wananchi kuona timu yao inapata mafanikio makubwa katika soka barani Afrika
Ukubwa wa klabu haupatikani kwa maneno tu bali vitendo vinapaswa kudhihirisha hilo
Yanga tayari imedhimirisha ukubwa wake kwenye soka la ndani na sasa ni muda wa kutafuta ukubwa katika ngazi za Kimataifa
Msimu huu Wananchi wako tayari na wana kila sababu ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa, Al Hilal hawapaswi kutoka salama watakapokuja jijini Dar es salaam