Ruvu Shooting mikononi mwa Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2022
Ruvu Shooting mikononi mwa Fei Toto

Habari njema kwa Yanga ni kurejea kikosini kiungo mshambuliaji Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye alitumia mapumziko ya kalenda ya FIFA kutibu majeraha aliyopata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zalan Fc

Lakini hii ni habari mbaya kwa Ruvu Shooting kwani kesho Jumatatu huenda wakakumbana nae pale dimba la Mkapa katika mchezo wa ligi kuu kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga

Fei Toto ana rekodi ya kipekee katika mechi alizokutana na Ruvu Shooting, takwimu za kuanzia mwaka 2018, amefunga mabao manne

Bao lake la nne lilikuwa msimu uliopita pale uwanja wa Benjamin Mkapa akiirejesha Yanga mchezoni kwa shuti kali kutoka umbali wa takribani mita 30

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mabao mengine yakifungwa na Djuma Shaban na Mukoko Tonombe

Msimu mmoja nyuma, Fei Toto aliwatungua Ruvu Shooting mabao mawili katika mchezo wake wa kwanza ambao kocha Nasreddine Nabi alianza kumtumia nafasi ya kiungo mshambuliaji

Msimu wa 2018/19 Fei Toto alifunga bao la ushindi kwa Yanga kwenye dakika za majeruhi katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1

Jumatatu anakutana na Ruvu Shooting, je ataendeleza rekodi ya kuwaadhibu maafande?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’