Yanga imeendeleza ubabe wake mbele ya Ruvu Shooting leo ikipata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ililazimika kusubiri mpaka kipindi cha pili kujihakikishia ushindi kwa mabao ya Feisal Salum 'Fei Toto' na nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto
Uzembe katika eneo la ulinzi uliigharimu Yanga kwenye dakika ya 85 kwa Msonjo kufunga bao la kufutia machozi kupitia mpira wa kona ambao ulimgonga Joyce Lomalisa na kutua mguuni kwa Msonjo
Ushindi huo umeirudisha Yanga kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 13 sawa na Simba, lakini wakitofautiana mabao
Yanga sasa inaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumamosi


ADVERTISE HERE