Afisa Habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji wa timu hiyo wanajifua kwa ari kubwa kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumamosi, Oktoba 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kamwe amesema ameshuhudia ari na morali ya aina yake katika viunga vya Avic Town, Kigamboni
Amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri mpaka sasa hakuna mchezaji majeruhi
"Tunashukuru hali ya kambi mpaka sasa iko vizuri, tunasema dalili ya mvua ni mawingu, huwezi kuamini mpaka sasa ndani ya kambi hakuna majeruhi hata mmoja na ukitaka kuamini wachezaji wanaitamani vipi Al Hilal, Stephane Aziz-Ki alipotua tu jana, akaelekea moja kwa moja mazoezini"
"Tunawaomba mashabiki waje kwa wingi Jumamosi, hii ni siku kubwa kwetu, siku ambayo tumedhamiria kwenda kuandika historia kubwa ya klabu yetu kwa kurejea kibabe hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa," alisema Kamwe