Wananchiiii, ni siku mbili tu zimesalia kuelekea lile jambo kubwa la kuirejesha heshima ya Yanga Kimataifa
Ni mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal, dakika 90 muhimu kwa Yanga kutafuta ushindi mnono kabla ya kusafiri kule Sudan kwenda kumaliza kazi wiki ijayo
Iwe Jua, Iwe Mvua lazima tuwapige kama ngoma! Kama bado hujakata tiketi, hakikisha unatumia vyema siku ya leo na kesho kujipatia tiketi yako
Kwa wale ambao wako jijini Dar es salaam na hawana uwezo wa kununua tiketi, Jimmy Kindoki majira ya saa tatu asubuhi atakuwa Makao Makuu ya klabu ya Yanga kugawa tiketi
Kindoki pia atafanya zoezi hilo kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Magufuli Stand
Tiketi ya Mzunguuko bado inapatikana kwa Tsh 3,000/- lakini ikifika Jumamosi tiketi hiyo utaipata kwa Tsh 5,000/-
Wapinzani wa Yanga Al Hilal wanatarajiwa kuwasili nchini jioni ya leo kuelekea mtanange huo ambao bila shaka Wananchi wataisimamisha nchi siku ya Jumamosi
