Keshokutwa Jumamosi Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Hilal katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga iliyo na mkakati wa kutinga hatua ya makundi baada ya kukosa kushiriki hatua hiyo kwa takribani miaka 24
Mashabiki wa Yanga wana matumaini makubwa kwa timu yao kuelekea mchezo huo ambao utapigwa majira ya saa kumi jioni
Wakati lengo la Yanga ni kushinda, lakini ni muhimu sana kwa Yanga kupata ushindi pasipo kuruhusu bao
Al Hilal walifuzu raundi ya kwanza kwa bao la ugenini, walifungwa mabao 2-1 na St George huko Ethiopia na wakashinda bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa Sudan
Safu ya ulinzi ya Yanga itapaswa kuwa makini ili kuhakikisha Al Hilal hawafungi bao hapa nyumbani
Kwa utamaduni wa timu za Arabuni huanza kwa kasi ugenini kusaka bao mapema na kama wakifanikiwa basi watatumia kila aina ya mbinu kupooza mchezo na kupoteza mda
Hivyo hawapaswi kupata fursa hiyo, na itakuwa muhimu kwa Yanga kufunga bao mapema ili kuwa na utawala wa mchezo