Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka wale ambao bado hawajakata tiketi kutumia muda uliobaki kabla ya kesho kununua tiketi zao
Kamwe amesema tiketi za Mzunguuko zitauzwa Tsh 5,000 siku ya kesho hivyo ni vyema kununua tiketi leo kwa Tsh 3,000/-
"Tunaomba mashabiki wetu mnunue tiketi mapema ili kesho tuwe na jambo moja tu, tukiamka asubuhi tunamshukuru Mwenye ez Mungu halafu tunakunywa chai kisha tunaelekea uwanja wa Benjamin Mkapa"
"Tumeagiza viongozi na mashabiki wote tunapaswa kuja uwanjani na jezi ya Yanga hatutaki kuona mtu amevaa suti. Tutaifundisha Afrika jinsi tunaweza kushangilia kistaarabu kuanzia dakika ya kwanza mpaka dakika ya 90"
"Tutahesabu mabao baada ya dakika 90, tunataka kuona shangwe kutoka kwa mashabiki kwa dakika zote za mchezo," alisema Kamwe
Katika hatua nyingine, Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine ametangaza kuwa klabu hiyo imeingia makubaliano na Smile Communications Tanzania Ltd kuwa washirika kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Al Hilal Club utakaochezwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa hapo kesho