Mtandao wa Foot Afrika umemtangaza mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele kuwa mchezaji bora wa Afrika mwezi Septemba 2022
Mayele ameshinda tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura kwa wingi na mashabiki wa soka barani Afrika
Amemshinda Baulaye Dia mshambuliaji wa Kimataifa wa Senagal aliyekuwa akichuana nae kwa ukaribu
Mayele amepata asilimia 37 ya kura zote zilizopigwa wakati Dia akipata asilimia 34
Mayele amekuwa na msimu mzuri mpaka sasa akifunga mabao saba kwenye mechi za hatua ya awali ligi ya mabingwa huku akiweka kambani mabao matatu katika mechi za ligi kuu
Pia alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na hivyo kuwa amefunga mabao 12 katika mashindano yote
ADVERTISE HERE