Wembe ni uleule hadi St Louis

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2018
Wembe ni uleule hadi St Louis
Baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji jana, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuandoka Jumapili kwenda Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya St Louis.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumatano February 21.

Msafari wa watu 30, ukijumuisha wachezaji 20, na viongozi 10 unatarajiwa kusafiri kwenda Shelisheli.

Matokeo ya mchezo wa kwanza hayakufurahiwa na wengi kwani ilitarajiwa Yanga kuibuka na ushindi mnono zaidi ya bao 1-0.

Benchi la Ufundi limesema watahakikisha Yanga inamaliza kazi ugenini.

Yanga inakwenda mapema Shelisheli ili kupata muda wa kuzoea hali ya hewa ambayo inaelezwa kuwa ni joto kali wakati huu.

Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuwa tofauti na uliochezwa jijini Dar es salaam ambao wenyeji walipaki basi kwa muda mwingi huku wakitumia mashambulizi ya kushitukiza.

Kwa kuwa Yanga tayari ina bao moja, wenyeji wao watalazimika kutafuta bao la kusawazisha na hata kufunga mabao zaidi kama watakuwa na lengo la kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Hiyo itatoa nafasi kwa Yanga nayo kuwashambulia na pengine kupata bao la ugenini litakaloigharimu zaidi St Louis.

Kama Yanga itafunga hata bao moja ugenini, St Louis watahitaji kufunga mabao matatu ili waweze kufuzu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’