Tunayo nafasi Sudan - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Oct 2022
Tunayo nafasi Sudan - Zahera

Mkurugenzi wa soka la Vijana Yanga Mwinyi Zahera amesema wanapaswa kwenda Sudan wakiwa na malengo ya kupata ushindi na sio vinginevyo

Zahera amewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2018/19 akiiongoza Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kumbukumbu kubwa ikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Township Rollers ya Botswana baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Zahera amesema Yanga na Al Hilal zinakaribiana kiuwezo hivyo bado wana nafasi ya kufanya vizuri huko Sudan kama ilivyo kwa wapinzani wao

"Huwezi kusema mchezo umekwisha hapa kwa sababu tumepata sare, tunasema Al Hilal wanafaida tu lakini bado hawajatushinda. Yanga inapaswa kwenda Sudan ikiwa na malengo sawa na waliyokuwa nayo hapa, kusaka ushindi"

"Hatupaswi kwenda na dhamira ya kuzuia, umeona jinsi tulivyocheza hapa kipindi cha kwanza, tulikuwa na tahadhari kubwa lakini kipindi cha pili tulipofunguka tuliweza kufunga ingawa yapo makosa wachezaji wetu walifanya," alisema Zahera

Aidha akizungumzia matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Hilal, Zahera amesema wachezaji waliathiriwa na presha ya nje ya uwanja na hivyo kusahau majukumu yao uwanjani

"Baada ya kufunga bao wachezaji wetu walijisahau na kuruhusu presha ya nje iwaingie vichwani. Kila mmoja alikuwa akifikiria kuwa tunapaswa kupata ushindi wa mabao mengi. Utaona baada ya kufunga bao tulifanya mashambulizi mengi langoni mwa Al Hilal kwa sababu idadi kubwa ya wachezaji wetu walikuwa wakisogea mbele kushambulia"

"Hapa ndipo tulipofanya kosa kwani asilimia 70 ya mabao Al Hilal wanafunga kupitia mipira ya kushitukiza kwa sababu wana wachezaji wenye mbio. Viungo wetu wote Aucho, Feisal na Aziz Ki hawakuwa katika maeneo yao tulipopoteza mpira. Al Hilal walitumia mapungufu hayo kutushambulia haraka"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’