Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema benchi la ufundi linatambua ugumu wa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumapili Oktoba 16 nchini Sudan
Hata hivyo amesema Yanga inafanya maandalizi ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri yatakayowawezesha kutinga hatua ya makundi
Bosi huyo wa kitengo cha Habari na Mawasiliano, amesema Yanga iliingia kambini tangu Jumatatu na watakamilisha maandalizi yao kesho Ijumaa kabla ya safari ya Sudan Jumamosi Alfajiri
ADVERTISE HERE