Mwanachama/Mhasishaji wa Yanga Haji Manara amesema ana imani kubwa Yanga inaweza kwenda kuwashangaza wengi kule Sudan kwa kupata ushindi dhidi ya Al Hilal
Yanga itasafiri Sudan kwenda keshokutwa Jumamosi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumapili Oktoba 16
Manara amesema haamini kikosi hiki cha Yanga hakitaweza kupata matokeo Sudan
"Mioyo yetu nadhani inatofautiana au labda mimi naangalia mpira tofauti na watu wengi. Narudia, ntakuwa mtu wa mwisho kuamini kikosi hiki kitatolewa na Al Hilal, najua leo kwa baadhi yenu ni ngumu kunielewa, ila naamini Wananchi tutafuzu Kwa Group Stage Insha'Allah," aliandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Yanga itakwenda Sudan ikiwa na rekodi ya aina yake, wakicheza zaidi ya siku 500 pasipo kupoteza mchezo wowote wa kimashindano
Kwa wachezaji wa Yanga sio suala la kulinda heshima na rekodi tu, lakini wana jukumu la kudhihirisha kuwa wao ni kizazi bora cha wachezaji waliopita Yanga