Ibenge ataonja dawa yake mwenyewe Sudan

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
13 Oct 2022
Ibenge ataonja dawa yake mwenyewe Sudan

Jumapili majira ya saa 2 usiku Yanga itashuka uwanja wa Al Hilal kule Sudan kuwakabili wenyeji wao katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika

Sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, unawapa faida Al Hilal ya bao la ugenini

Hivyo ni lazima Yanga ikalitafute bao hilo kule Sudan kuweka mambo sawa kabla ya kutafuta mabao mengine ili kushinda mchezo huo

Kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, presha ilikuwa kwa upande wa Yanga iliyocheza mbele ya takribani mashabiki 45,000 waliojitokeza kuishangilia timu yao

Kocha Mkuu wa Al Hilal Florent Ibenge alifanikiwa kuwatuliza vijana wake na wakacheza vizuri mchezo huo wakitumia vyema dakika 30 za mwisho ambapo walifanikiwa kusawazisha bao na kutengeneza nafasi nyingi

Al Hilal hawakuwa na umiliki wa mchezo, waliwaachia Yanga wacheze lakini walitumia mashambulizi ya kujibu kila Yanga walipopoteza mpira katika lango lao

Katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa uwanja wa Al Hilal siku ya Jumapili, itakuwa zamu ya kocha Nasreddine Nabi kutumia mazingira hayo kuipa Yanga matokeo

Hakuna shaka mashabiki wa Al Hilal watafurika katika uwanja wao na hakuna kitu watahitaji zaidi ya kuona timu yao inaibuka na ushindi mnono, kama ilivyokuwa kwa mashabiki wa Yanga hapa jijini Dar es salaam

Silaha ambayo Ibenge aliitumia katika dimba la Benjamin Mkapa ndio silaha ambayo Nabi atapaswa kuitumia kule Sudan

Huu ni mchezo ambao Yanga inahitaji kushambulia kwa kujibu 'counter-attack' kama walivyofanya Al Hilal hapa Tanzania

Mara nyingi timu inapocheza nyumbani inaamini kuwa na haki ya kupata ushindi hivyo Al Hilal watajaribu kusaka ushindi kwa gharama yoyote hasa ikizingatiwa wanacheza mbele ya mashabiki wao

Hizi ni aina ya mechi ambazo wachezaji wenye kasi kama Fiston Mayele, Bernard Morrison, Tuisila Kisinda, Stephane Aziz Ki kasi yao inaweza kuwa na faida kubwa kwa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’