Ni mechi kubwa, mechi ya heshima kwa Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Oct 2022
Ni mechi kubwa, mechi ya heshima kwa Wananchi

Ni siku mbili zimesalia kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa mkondo wa pili dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Jumapili, Oktoba 16 huko nchini Sudan

Mechi kubwa, mechi ya heshima kwa Wananchi, thamani ya ushindi wanaoweza kupata wachezaji wa Yanga, ni matokeo ambayo yatabaki mioyoni mwa Wananchi na hakuna shaka yataingia katika vitabu vya kumbukumbu vya klabu ya Yanga

Achana na bonus na zawadi ambazo wachezaji wa Yanga watapata kama watafanikiwa kupata ushindi, lakini kubwa zaidi ni kulinda heshima na kuipaisha Yanga Kimataifa

Al Hilal wanashika nafasi ya 12 katika viwango vya ubora wa klabu barani Afrika, kama Yanga itaweza kuwaondosha kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kutinga hatua ya makundi, itaongeza pointi nyingi na kupanda juu katika viwango vya ubora

Kwa uwekezaji uliofanywa na GSM, huu ni msimu ambao Yanga inastahili kucheza hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa

Wachezaji wa Yanga wanafahamu wanakwenda vitani huko Sudan, wakirejea na ushindi majina yao yataandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye mioyo ya Wananchi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’