Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanakwenda Sudan kwa lengo moja la kusaka ushindi dhidi ya Al Hilal ili kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Nabi amesema wamefanya maandalizi ya kutosha, morali ya wachezaji iko juu na wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo
Amesema katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam walikosa bahati tu lakini walicheza vizuri
"Tunajua Al Hilal ni timu nzuri lakini nasisi tuna timu nzuri. Hatukushinda mchezo wa kwanza tulikosa bahati tu lakini tulikuwa na dakika 65 nzuri. Tunawaahidi mashabiki wetu tunakwenda Sudan kupambana na Inshalla tutarejea na ushindi siku ya Jumatatu"
"Nimewaambia wachezaji wangu wasiwe na hofu yoyote, tunakwenda kucheza kwenye uwanja mzuri wa Al Hilal. Mashabiki wao watakuwa wengi uwanjani lakini sisi tuna wachezaji ambao wana uzoefu wa kucheza katika mazingira ya aina hiyo"
"Kikubwa tunaomba mashabiki wetu watuombee na kwa upande wetu tumejipanga kuwapa furaha Jumapili Inshallah," alisema Nabi