Droo ya raundi ya mtoano kombe la Shirikisho barani Afrika inafanyika kesho Jumanne ambapo Yanga itakuwa na nafasi nyingine kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi
Yanga ilipoteza mchezo dhidi ya Al Hilal kwa kufungwa bao 1-0 jana na hivyo kuondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa kwa kipigo cha mabao 2-1
Yanga haikuondoshwa kinyonge kwani wachezaji walipambana na pengine hawakustahili matokeo hayo
Hata hivyo ndivyo ilivyo zinaposhindana timu mbili lazima mshindi awe mmoja na mwingine ajifunze
Yanga inakwenda Shirikisho ikifahamu nini inapaswa kufanya hasa katika uwanja wake wa nyumbani
Sio rahisi kupata ushindi ugenini hasa unapokutana na timu hizi za kiarabu katika hatua ya mtoano
Wenzetu wanajua kutengeneza mazingira ya kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani
Wanajipanga nje na ndani ya uwanjani, swali ambalo wananchi tunapaswa kujiuliza ni kwa nini sisi hatuwezi kutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo?
Imekuwa hivi kwa Yanga katika michuano ya Kimataifa, kwa soka la Afrika haipaswi kuwa hivi