Rostand tayari kurejea kikosini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
17 Feb 2018
Rostand tayari kurejea kikosini
Kipa wa Yanga, Youthe Rostand, amethibitisha kuendelea vizuri akirejea sasa katika ukakamavu huku akiwa ameshaanza kufanya mazoezi na wenzake na kusema siku chache zijazo mashabiki watamuona uwanjani.

Rostand aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli mwezi huu, hivyo kuliacha lango la timu hiyo kwa chipukizi, Ramadhani Kabwili ambaye hata hivyo anafanya vizuri.

Kipa huyo raia wa Cameroon amesema alikaa nje baada ya kuambiwa apumzike na daktari, lakini sasa anafanya mazoezi na wenzake.

“Nimeshaanza mazoezi, lakini nimeambiwa niwe napumzika ili niwe fiti zaidi na kuitumikia timu yangu katika mashindano,” alisema.

“Unajua unapotoka benchi la majeruhi inahitaji upate muda wa kurejea taratibu usije ukaumia zaidi.

“Sina tatizo lingine lolote zaidi ya lile la majeruhi, kukosekana kwangu katika mechi za kimataifa ni kwa sababu naumwa, ndio maana hata katika mechi za ligi pia nimekosekana.”

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →