Mfalme wa mechi za dabi ni mmoja tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Oct 2022
Mfalme wa mechi za dabi ni mmoja tu

Jumapili Yanga itaingia uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watani zao Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC. Ni mchezo wa kwanza wa dabi kwenye ligi msimu huu

Lakini pia utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo katika msimu huu ukitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Yanga ilishinda mabao 2-1

Zinapokuja mechi za dabi, Yanga ndiye mfalme wa mechi hizi ikipata ushindi mara nyingi kuliko watani zao

Ni takribani miaka mitatu sasa Simba haijaonja radha ya ushindi mbele ya Yanga katika mechi za ligi kuu

Februari 16 2019 ndio mara ya mwisho kwa Simba kushinda mchezo wa ligi kuu mbele ya Yanga, wakati huo Wananchi wakinolewa na Kocha Mwinyi Zahera

Tangu wakati huo, zimechezwa mechi sita za ligi, Yanga imeshinda mechi mbili na mechi nne kumalizika kwa matokeo ya sare

Katika mechi tano zilizopita kwenye mashindano yote, Yanga imeshinda tatu na mechi mbili kumalizika kwa sare

Ni rahisi kuelewa kwa nini mashabiki wa Simba kwa sasa tambo zao wamezielekeza Kimataifa zaidi na msemo wao siku hizi wanasema Yanga huwa wanakamia mechi za dabi ndio maana wanashinda sana!

Yanga ina kawaida ya kufanya vizuri katika mechi hizi bila ya kujali mazingira wanayopitia au aina ya kikosi walichonacho

Wakati huu Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na mahitaji ya ushindi zaidi pengine kuliko ile mechi ya Ngao ya Jamii

Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kuangukia kombe la Shirikisho, wachezaji wa Yanga wanafahamu ushindi katika mchezo huo utarejesha tabasamu katika nyuso za mashabiki wao na kuwaongezea morali kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’