Nyota wa zamani wa Yanga, Mrundi Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ ambaye kwa sasa anakipiga Geita Gold ameweka wazi tofauti zilizopo kati ya chama lake hilo la zamani na timu nyingine za Ligi Kuu
Saido ameeleza Yanga ina utofauti mkubwa na timu nyingine kutokana na namna inavyoendeshwa, uchezaji wake na mazingira ya wachezaji kuwa tofauti na hilo ndilo linaifanya iendelee kuonekana kubwa
"Unaweza kusema timu zote ni sawa kwa kuwa zinacheza ligi moja, lakini ndani yake kuna utofauti mkubwa karibu wa kila kitu," alisema Saido aliyeichezea Yanga msimu uliopita
"Siwezi kuizungumzia sana Yanga kwa kuwa sasa nipo na timu nyingine, kipindi nipo pale mambo mengi yalikuwa ya kipekee na kwa ukubwa na ubora tofauti na timu nyingine zinavyoishi," Saido aliliambia gazeti la Mwanaspoti
Saido aliondoka Yanga katika dirisha la usajili lililopita baada ya kushindwa kufikia makubaliano na uongozi kuhuisha mkataba wake uliokuwa umemalizika