Ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 19 imeendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya Lipuli FC dhidi ya Azam FC kupigwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Iringa
Mchezo huo umemalizika kwa suluhu ya 0-0 hivyo kuifanya Azam FC iendelee kubaki nafasi ya tatu baada ya kufikisha alama 35.
Azam FC ilianza msimu kwa kishindo lakini sasa inaonekana wameanza kuishiwa na pumzi ya kupambana na wakongwe Simba na Yanga walio nafasi za juu.
Hata hivyo duru ya pili ligi kuu ya Vodacom huwa ina kawaida ya kuwa na ugumu kwa kuwa ukiachilia mbali timu zinazowania ubingwa, kuna timu nyingi zinapambana zisiteremke daraja.

ADVERTISE HERE