Mwanachama na aliyekuwa Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema Yanga inauchukulia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba kwa uzito na umuhimu mkubwa wakitambua ni mchezo wa dabi ambao ushindi wake una heshima na unapeleka furaha kwa mashabiki wao
Manara amewashukia baadhi ya wachambuzi wanaotumika kueneza propaganda kuwa Simba haichukulii kwa uzito mkubwa mchezo huo kwa kuwa sio muhimu kwao kwa vile malengo yao ni michuano ya Kimataifa zaidi
Manara amesema propaganda hizo ni mbinu inayotumiwa na watani zao kujihami baada ya kuona imekuwa sio rahisi kwao kupata ushindi dhidi ya Yanga licha ya kila mbinu walizotumia
Manara ametamba kuwa wataendeleza ubabe wao dhidi ya Simba kwa kupata ushindi siku ya Jumapili
ADVERTISE HERE