Nabi aomba radhi, aahidi ushindi dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Oct 2022
Nabi aomba radhi, aahidi ushindi dhidi ya Simba

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kushindwa kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika

Nabi ameahidi kuwapa furaha kwa timu yake kupata matokeo mazuri katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Nabi amesema maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba yamekamilika wakiwa wamejipanga kushinda mchezo huo

"Nawaomba radhi mashabiki wa Yanga kwa kushindwa kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa, nashukuru kwa upendo walionionyesha pamoja na kuniunga mkono kwani wapo ambao walitamani kuona nadondoka lakini haikuwa hivyo"

"Tumejiandaa vizuri kwa mchezo dhidi ya Simba, wachezaji wako tayari naamini tutapata matokeo mazuri," alisema Nabi

Akizungumzia utayari wa wachezaji kuelekea mchezo huo, Nabi amesema Bernard Morrison ndiye mchezaji ambaye atakosekana akitumikia adhabu wakati hatma ya Salum Abubakar 'Sure Boy' itategemea na mazoezi ya leo

"Morrison anatumikia adhabu wakati Sura Boy ametoka katika ugonjwa hivyo tutaangalia utayari wake katika mazoezi ya mwisho leo. Wachezaji wengine wote wako tayari"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’