Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba hapo jana, Yanga haina muda wa kupoteza kwani wana siku mbili kabla ya kurudi tena uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili KMC
Inaweza kuwa wiki ya bandika bandua kwa Yanga kwani kama hakutafanyika mabadiliko ya ratiba, baada ya mchezo dhidi ya KMC, Yanga itasafiri jijini Mwanza kuikabili Geita Gold katika mchezo mwingine utakaopigwa Oktoba 29
Wananchi wanapaswa kuwa Dar Novemba 02 kuikabili Club Africain kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza mtoano kombe la Shirikisho kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi
Kwa sasa Kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi wanaelekeza nguvu katika mchezo unaofuata dhidi ya KMC
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo kwani sasa Wananchi sasa wamecheza mechi tatu mfululizo pasipo kupata ushindi