Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana kwa Yanga jana lakini umahiri wa Stephane Aziz Ki uliihakikishia Yanga kurudi mchezoni kwa bao lake la mpira wa adhabu katika dakika ya 45 kufanya ubao usomeke 1-1
Yanga ikarejea ikiwa imara zaidi kwenye kipindi cha pili lakini bahati haikuwa upande wa Wananchi kwani licha ya nafasi kadhaa walizotengeneza, hawakuweza kutumbukiza mpira kimiani
Kuna watu walianza kusahau ubora wa Aziz Ki lakini jana amewakumbusha Aziz Ki ni yule yule
Lile goli alilomfunga Manula angeweza kufungwa kipa yeyote hata kipa bora wa dunia Thibaut Courtois wa Real Madrid hadaki ile!
Huyu Ki amemfunga Manula mabao matatu. Wakati yuko Asec Mimosas alimtungua mabao mawili
Sasa amefikisha mabao mawili na asisti moja katika ligi kuu ya NBC
Yawezekana mwanzo wake na Yanga sio bora sana lakini taratibu ameanza kuonyesha ni kwa kiasi gani ni mchezaji wa daraja la juu