Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amekanusha tetesi zinazoihusisha timu hiyo kuachana na kocha wake mkuu Nasredine Nabi
Mtine amewataka Mashabiki na Wanachama wa Yanga wasikubali kuyumbishwa na taarifa za upotoshaji, kutoka katika vyanzo ambavyo sio rasmi
Aidha uongozi wa Yanga umemtakia kila la kheri Nabi na benchi lake la ufundi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga imewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji wao katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja usiku
ADVERTISE HERE