Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza na wanahabari katika mkutano maalum wa mechi, Nabi amesema wanakwenda kukabiliana na KMC ambayo iko katika kiwango bora sana msimu huu
"KMC imezidi kuwa na ubora zaidi hususani msimu huu kutokana na ubora walioonyesha kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc pamoja na Simba, tunawaheshimu lakini tumejiandaa vizuri kuwakabili," alisema Nabi
Aidha Nabi amesema licha ya kupata siku mbili tu kujiandaa na mchezo huo, wataingia dimbani wakiwa na dhamira moja ya kuibuka na ushindi
"Tutazingatia utayari wa kila mchezaji hasa ikizingatiwa tumetoka kucheza mechi ngumu, kama kutakuwa na ulazima wa kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya maeneo tutafanya lakini jambo muhimu kwetu ni kupata ushindi bila ya kujali nani atacheza"