Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi wanapambana kulinda afya za wachezaji kutokana na changamoto ya ratiba
Yanga itacheza mechi nne katika kipindi cha siku 12 ambapo ni wastani wa kucheza mechi kila baada ya siku tatu
Oktoba 23 Wananchi walicheza na Simba mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Jana Oktoba 26 Yanga ikarudi tena uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili KMC katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0
Katika mchezo wa jana, Nabi alilazimika kufanya mabadiliko ya kikosi akiwapa mapumziko baadhi ya wachezaji kama Djuma Shaban, Fiston Mayele, Kibwana Shomari, Khalid Aucho ambaye pia alikuwa na kadi tatu za njano
Baada ya mchezo huo, Yanga inasafiri kuelekea jijini Mwanza wanakokabiliwa na mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold Oktoba 29
Wakimalizana na Geita Gold Wananchi hawatapumzika kwani wanapaswa kurejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kusaka kutinga makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ambao utapigwa Novemba 02
Ni wazi katika mchezo dhidi ya Geita Gold Nabi atalazimika kuchukua tahadhari nyingine kwa wachezaji wake muhimu ili kuhakikisha anakuwa kikosi chake kamili atakapowakabili Club Africain