Ikiwa sehemu ya makubaliano ya Mkataba kati ya Yanga na Shirika la Umoja wa Mataifa la Unicef uliosainiwa hivi karibuni, uongozi wa Yanga umetangaza utaratibu wa kugawa tiketi kwa mashabiki 10,000 kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ambao utapigwa Novemba 02. Tiketi hizo zitagaiwa kwa wale wataopata chanjo ya Uviko 19
Wakizungumza na wanahabari mapema leo Mtendaji wa Yanga Andre Mtine na Mtendaji wa Jackson Group Kelvin Twissa, wamewema utaratibu umeandaliwa kuwafikia Wananchi mitaani ili toa elimu ya ebola na chanjo ya uviko 19
Baadhi ya viongozi wa Yanga, wachezaji na maafisa wengine waandamizi watashiriki kutoa hamasa ya chanjo ya Uviko 19 na elimu ya virusi vya Ebola
Hii ni nafasi ya adimu kwa Wananchi kupata chanjo ya Uviko 19 bure, pia pamoja na tiketi ya kushuhudia mchezo dhidi ya Club Africain, utapata jezi, kofia na fursa ya kuwaona wachezaji pendwa wa Yanga pamoja na kupiga picha na makombe yote