Makambo ana kazi ya kufanya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2022
Makambo ana kazi ya kufanya

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amekiri mshambuliaji Heritier Makambo alikuwa chini ya kiwango katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold

Hata hivyo Kaze amesema walilazimika kumtumia Makambo ili kumpumzisha Mayele ambaye alipata majeraha wakati wakijiandaa na mchezo dhidi ya KMC

"Ni kweli Makambo hakuwa katika kiwango bora leo lakini ilikuwa ni lazima tumtumie ili kumpa Mayele mapumziko. Mpango ulikuwa kumpa Mayele muda wa kucheza usiozidi dakika 25, anarejea kutoka kwenye majeruhi na tutahitaji kumtumia katika mechi ijayo," alisema Kaze

Katika mechi mbili dhidi ya KMC na Geita Gold, Makambo amekosa umakini ambapo ameshindwa kutumia nafasi kadhaa za wazi

Makambo alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga, lakini sasa anahitaji kufanya kazi ya ziada katika viwanja vya mazoezi ili kurejea katika ubora wake wa zamani

Ikumbukwe Yanga itaongeza nguvu kwenye dirisha dogo, Yacouba Songne yuko tayari kurejea baada ya kupona majeraha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’