Club Africain wanafungika - Kocha Kipanga Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Nov 2022
Club Africain wanafungika - Kocha Kipanga Fc

Kocha Mkuu wa Kipanga FC ya Zanzibar, Hassan Abdulrahman amesema Yanga inaweza kuwaondoa Club Africain kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kama watakuwa na umakini katika mechi zote mbili

Kipanga Fc ilikutana na Club Africain katika michuano hiyo hatua iliyopita ikipoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 7-0

Mchezo wa kwanza uliopigwa visiwani Zanzibar ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana na Kipanga wakapoteza ugenini kwa kufungwa mabao 7-0

Abdulrahman amesema Club Africain hawachezi soka la nguvu sana lakini wako makini sana katika kutumia nafasi wanazotengeneza

"Yanga wanapaswa kucheza na timu hii kana kwamba hawaifahamu, wasichukue matokeo yetu tuliyopata hapa Zanzibar na kule kwao. Mchezo wao utakuwa tofauti"

"Sisi ni timu changa, hii ni mara yetu ya pili kushiriki michuano ya CAF hivyo hatukuwa na uzoefu na mashindano haya. Lakini ni tofauti kwa Yanga wao wanataka kushinda ili kutinga makundi na hata Club Africain ni hivyohivyo"

"Ubora wa Club Africain uko katika eneo la kati na walinzi wa pembeni. Wao wanacheza mfumo wa 3-5-2, wanatumia mabeki wao wa pembeni kushambulia. Walitumia mfumo huo katika mechi zote mbili tulizocheza nao," alisema Abdulrahman

Aidha mkufunzi huyo wa Kipanga amesema hali ya hewa ya mji ambao Club Africain wanatoka haina tofauti na hali ya hewa ya Dar es salaam na hata uwanja wanaotumia ni wa nyasi asilia kama ulivyo uwanja wa Benjamin Mkapa

"Tulipokwenda Tunisia hujuma waliyotufanyia ni kutunyima kufanya mazoezi katika uwanja uliotumika, tuliouona kwa macho tu. Lakini hali ya hewa haikuwa kikwazo, uwanja wao ni wa nyasi asilia kama ulivyo uwanja wa Mkapa. Tulipoteza mchezo kwa kuwa vijana wetu hawana uzoefu na mashindano haya pamoja na kukosa umakini"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’