Mlinzi wa kulia wa Yanga Djuma Shaban sio miongoni mwa wachezaji waliosafiri jana kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain. Mchezo huo utapigwa Jumatano, Novemba 09 huko jijini Tunis
Djuma alipata majeraha ya nyama za paja katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Club Africain uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumatano iliyopita na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi atamrudisha Kibwana Shomari upande wa kulia na pengine kwenye safu ya ulinzi upande wa kushoto atamtumia Farid Mussa

Baada ya Djuma kuumia katika mchezo uliopita, Farid aliingia na kucheza beki wa kushoto wakati Kibwana akihamia upande wa kulia
Yanga inahitaji kupata ushindi au matokeo ya sare ya mabao ili kuweza kutinga hatua ya makundi
Hakuna jambo lisilowezekana kwenye mpira wa miguu