Manji bado ni mgonjwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
19 Feb 2018
Manji bado ni mgonjwa
Afya ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji bado haijaimarika vizuri baada ya kulazimika kufanyiwa upasuaji mwingine mdogo na kuwekewa chuma katika mshipa mmoja wa damu.

Kulingana na gazeti la Champion, mwezi uliopita, Manji alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kufanyiwa upasuaji huo mdogo.

Kutokana na upasuaji huo, Manji amewekewa vyuma viwili ndani ya mwaka mmoja tangu ashitakiwe kwa tuhuma ya matumizi ya dawa za kulevya. Alifanyia upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Kulingana na gazeti hilo, madaktari wameeleza si salama kwa Manji kufanyiwa upasuaji wa namna hiyo ndani ya mwaka mmoja.

“Angalau miaka minne au mitatu, lakini yeye ni mwaka mmoja amewekewa vyuma mara mbili. Daktari ameonya kwamba si jambo jema kiafya,” kilieleza chanzo.

“Hata hivyo, wamekuwa wakifanya siri sana. Unajua amekuwa na presha sana kutokana na matatizo yanayomuandama. Kuna wafanyakazi zaidi ya 4,750 waliokuwa wanafanya kwa Manji ilibidi waondolewe maana kampuni zake zote zimefungwa.

“Hii inaonekana kumchanganya sana, ndiyo maana amekuwa akiumwa na alikatazwa hata kuzungumza na simu hadi wiki moja iliyopita.”

Juhudi za kumpata Manji zilifanyika na juzi jioni alipatikana, naye alipoulizwa akagoma kufafanua zaidi ya kuthibitisha kweli alilazwa.

“Ndiyo ninaumwa, nililazwa Aga Khan. Sasa mimi sipendi kuzungumza mambo yangu ya ugonjwa kwenye vyombo vya habari,” alisema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →